CHAMA CHA WAFANYAKAZI WA TAASISI ZA ELIMU YA

1y ago
47 Views
1 Downloads
422.72 KB
33 Pages
Last View : 8d ago
Last Download : 5m ago
Upload by : Audrey Hope
Transcription

CHAMA CHA WAFANYAKAZI WA TAASISI ZAELIMU YA JUU TANZANIA (THTU)RIPOTI YA KAMATI YA UCHAMBUZI NA USHAURIKUHUSU BAJETI KUU YA SERIKALI YA MWAKA WAFEDHA 2019/2020i

YALIYOMOYALIYOMOiiSHUKRANIiiiMUHTASARIivVIFUPISHO VYA MANENOviDIBAJIvii1UTANGULIZI12MIONGOZO MIKUU YA MAANDALIZI YA BAJETI1342.1Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 202512.2Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2015–202022.3Mpango wa Maendeleo wa Taifa3MWENENDO WA BAJETI YA TAIFA43.1Mchakato na Vipaumbele vya Bajeti43.2Sera, Mwenendo na Tathmini ya Bajeti53.3Vipaumbele Katika Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2019/2073.3.1Kilimo, Ufugaji na Uvuvi83.3.2Viwanda, Biashara na Uwekezaji83.3.3Miradi ya Miundombinu8MAPENDEKEZO YA UBORESHAJI WA BAJETI YA TAIFA94.1Utekelezaji wa Sera ya Viwanda4.2Uimarishaji wa Mapato Kuongeza Uwezo wa Serikali104.3Maboresho ya Mifumo ya Kukusanya Kodi134.4Kufungamanisha Ukuaji wa Uchumi na Maslahi ya Wafanyakazi174.5 Ushirikishwaji wa vyama vya Wafanyakazi katika mikakati mbalimbali9215HITIMISHO236REJEA23ii

SHUKRANIUchambuzi huu wa maandalizi ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2019/20 umeandaliwaili kuisaidia serikali, bunge na wadau wengine wa maendeleo katika kuandaa bajetiyenye tija itakayosaidia katika kufikia malengo ya uchumi wa kati unaotegemeaviwanda uliofungamanishwa na kuboresha maisha ya watanzania wakiwemowafanyakazi.Kwa niaba ya Uongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya JuuTanzania (THTU), shukrani za dhati ziende kwa kamati ya uchambuzi wa bajetiiliyohusisha wataalamu wanachama kutoka taasisi za elimu ya juu wakishirikiana nauongozi wa THTU Taifa katika mchakato wa kuchambua bajeti na kutoa mapendekezoya namna bora ya kuboresha bajeti ya nchi: Dkt. Paul Loisulie (THTU Makao Makuu),CPA Aisha Kapande (THTU Makao Makuu), Dkt. Alex Reuben Kira (UDOM), Dkt.Lutengano Mwinuka (UDOM), Ndg. Ngussa Kinamhala (CBE), Ndg. Deo Shao(UDOM), CPA David Mwakapala (UDOM), Ndg. Bonaventure Mshibika (IAA) na Ndg.Salum Hamisi (THTU Makao Makuu). Uchambuzi wa maandalizi haya ya bajetiumezingatia miongozo, sera, mipango na mikakati ya nchi na malengo mahususi yaTHTU.Zaidi ya hayo, uongozi wa THTU kwa ujumla unatambua mchango wa wanachamawake wote katika kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa ili kufikia malengoyanayotarajiwa kwa wakati. Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU), 2019Sehemu yoyote ya Ripoti hii inaweza kunakiliwa kwa matumizi yasiyo ya kibiashara,kwa sharti kwamba chanzo kitatambuliwa na nakala mojamoja ya chapisho itatumwakwa THTU.Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU)S.L.P 35928 DAR ES SALAAM, TanzaniaSimu: 022 2401581, Nukushi: 022 2401582Wavuti: www.thtu.or.tz, Barua pepe: [email protected]

MUHTASARIWafanyakazi ni wadau muhimu katika kujenga uchumi wa taifa. Kuna uhusiano wakaribu kati ya wafanyakazi na sekta nyingine zote katika uchumi. Kipato anachopatamfanyakazi aliyeajiriwa au kujiajiri kwa namna moja au nyingine kinagusa na kufikakatika maeneo tofauti kwa njia ya wao kukidhi mahitaji mbalimbali ya bidhaa nahuduma.Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 ilianza kutekelezwa mwaka 2000 ili kuongoza harakatiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii zitakazoiwezesha Tanzania kufikia uchumi wakati na kuondokana na umaskini uliokithiri ifikapo mwaka 2025. Katika kuchambuabajeti kuu ya serikali, Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 inaangazia malengo ambayo nikuhakikisha kuwepo kwa jamii iliyoeleimika vema na inayojifunza na kujenga uchumiimara unaoweza kukabiliana na ushindani kutoka nchi nyingine. Sambamba na hili,Ilani ya Chama cha Mapinduzi 2015-2020 pamoja na Mpango wa Maendeleo wa MiakaMitano (2016/17–2020/21) vinatoa vipaumbele katika kufikia malengo husika.Vipaumbele hivyo ni pamoja na ustawi wa wananchi; kuondoa umaskini nakupunguza tatizo la ukosefu wa ajira hasa kwa vijana; ukuaji wa uchumi (kufikiaasilimia 10); mfumuko wa bei (wastani usiozidi asilimia 5); na urari wa biashara naukuaji wa sekta ya kilimo.Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019 serikali imefanya juhudi katika kutafutambinu mbadala za kuongeza na kuimarisha mazingira ya kukusanya pato la ndani.Juhudi hizi zilijumuisha kufanya marejeo ya baadhi ya sheria za kodi ili ziwezekuendana na mazingira ya nchi yaliyopo. Malengo makuu ya kisera katika kuongezamakusanyo ya mapato ni pamoja na kupunguza misamaha ya kodi isiyo na tija,kuongeza utumiaji wa mifumo ya kielektroniki katika ukusaji wa mapato, kuendeleakuboresha usimamizi na ukaguzi kwenye mipaka ya nchi, bandari na viwanja vyandege, na kupanua wigo wa mapato.Hata hivyo, ufanisi wa makusanyo upande wa Serikali za Mitaa umekua duni katikakipindi kirefu sasa. Kwa mfano, kwa wastani wa kipindi cha miaka mitatu iliyopita niasilimia 79 tu ya makusanyo yalipatikana ikilinganishwa na lengo lililowekwa. Katikamapendekezo ya Mpango wa Maendeleo kwa mwaka wa fedha 2019/2020, serikaliimeainisha vyanzo mbalimbali vya mapato vinavyotazamiwa kugharimia shughuli zamaendeleo. Hata hivyo, mwenendo wa upatikanaji wa mapato ya utekelezaji wa bajetiunatia shaka katika kufikia lengo lililokusudiwa. Mathalani Katika kipindi cha mwakaiv

2016/2017 kati ya TZS trilioni 11.8 zilizotengwa kutekeleza miradi ya maendeleo nikiasi cha TZS trilioni 6.4 tu sawa na asilimia 55 ndicho kilipatikana katika kutekelezalengo. Vivyo hivyo, katika kipindi cha mwaka 2017/2018 ambapo kati ya TZS trilioni11.4 ni TZS trilioni 6.5 pekee sawa na asilimia 57 zilitolewa. Hali hii ya kushindwakutekelezeka kwa malengo ya mpango wa maendeleo inatokana na ukusanyaji hafifuwa mapato ya ndani na utegemezi wa fedha za mikopo na fedha za wafadhili kutokakwa wahisani.Ufanisi wa utekelezaji wa sera ya viwanda utasaidia sana kuongeza mapato ya serikalina hivyo kuiwezesha kuboresha maslahi ya wafanyakazi. Ili kufikia ufanisi huo, THTUinapendekeza namna bora zaidi ya kutekeleza sera ya viwanda ikiwa ni pamoja naUimarishaji wa Makusanyo Mapato ya ndani ikihusishakuongeza Uwezo wa Serikalikuibua na kubuni vyanzo vipya; Maboresho ya Mifumo ya Kukusanya Kodi hasakuimarisha matumizi ya TEHAMA; Kufungamanisha Ukuaji wa Uchumi na Maslahi yaWafanyakazi; mabadiliko katika Sheria za Kodi na muhimu zaidi Ushirikishwaji wavyama vya Wafanyakazi katika mikakati mbalimbali ya serikali.v

VIFUPISHO VYA MANENOASDP IIMpango wa Maendeleo ya Kilimo Awamu ya PiliCBEChuo cha Elimu ya BiasharaCCMChama Cha MapinduziFYDPMpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka MitanoGePGMfumo wa Malipo SerikaliniGOT-HOMISMfumo wa Kielektroniki wa Kuendesha HospitaliIAAChuo cha Uhasibu ArushaILOShirika la Kazi DunianiITUShirikisho la Mawasiliano la KimataifaLESCOBaraza la Kazi la Jamii na UchumiMKUKUTAMkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza UmaskiniTEHAMATeknolojia ya Habari na MawasilianoTHTUChama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu TanzaniaTRAMamlaka ya Mapato TanzaniaUDOMChuo Kikuu cha DodomaVATKodi ya Ongezeko la Thamanivi

DIBAJIKuhusu Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU)Chama cha wafanyakazi wa taasisi za elimu ya juu Tanzania (THTU) kimeanzishwakisheria kutetea uboreshaji wa maslahi mbalimbali ya wafanyakazi katika taasisi hizo.Utetezi huu unafanyika kwa mujibu wa sheria, kanuni, taratibu, miongozo na nyarakambalimbali za serikali au taasisi husika. Kauli mbiu ya THTU ni hii; Nia na Mwelekeoni Kujenga Daima, Taifa Kwanza.Kihistoria, uanzishwaji wa vyama vya wafanyakazi umejikita katika harakati zaidi nahivyo kujenga sura ya kutoaminiana kati ya mwajiri na wafanyakazikatika utekelezajiwa maslahi ya wafanyakazi. Mabadiliko ya kisheria, kimfumo na kimuundo yamekuwayakitokea katika uendeshaji wa vyama hivi na kupelekea kupungua kwa utamaduni wakutoaminiana uliokuwepo awali.Kutokana na mabadiliko hayo tajwa, uanzishaji wa THTU umejielekeza katikakuboresha mbinu za kutetea maslahi ya wafanyakazi. Kauli mbiu ya THTU ya Nia namwelekeo ni kujenga daima, Taifa kwanza imebuniwa kwa lengo la kutoa muelekeompya na mbinu za kisayansi katika kutetea maslahi ya wafanyakazi. Mbinu zakisayansi ni kufanya utafiti na kuonesha kitakwimu na kiuhalisia katika kujenga hojapamoja na kuishauri serikali namna bora ya kuimarisha uchumi na hatimae kuboreshamaslahi ya wafanyakazi. Sheria za Tanzania zimeweka utaratibu mzuri wa kuongozauendeshaji wa vyama vya wafanyakazi na namna ya kuwasiliana na mwajiri. Mfano wataratibu hizo zilizowekwa kisheria ni pamoja na majadiliano kazini, uanzishwaji wamabaraza ya wafanyakazi na uwakilishi wa wafanyakazi katika vyombo vya maamuzikwa kutaja machache. Kutokana na kauli mbiu ya THTU, tunaona tuna deni kubwakatika taifa hili kutoa mchango wetu kwa ustawi wake na kupata maendeleo endelevuna hatimae sisi wafanyakazi kunufaika moja kwa moja.Ni kwa msingi huo ulioelezwa hapo juu, THTU inaona ina wajibu wa kushirikikikamilifu katika ujenzi wa taifa hili katika kufikia malengo yanayotarajiwa kwawakati. Kauli mbiu hii inatuhamasisha sisi THTU kuwa washirika wa maendeleo nasi watazamaji. Hii maana yake ni kwamba tukishiriki kikamilifu katika kukuza pato lataifa, nasisi wafanyakazi tunafaidika moja kwa moja maana ni washirika. Katika dhanaya ushirika katika maendeleo, kila upande una kitu cha kuchangia kwa manufaa yapamoja.vii

Jambo moja muhimu la kuweka bayana ni kwamba THTU ina hazina kubwa yawanachama wenye viwango na weledi mkubwa wa elimu waliotabaharia/bobea katikanyanja mbalimbali. Ili kufikia azma ya kutetea uboreshwaji wa maslahi ya wafanyakazi,THTU imeunda kikosi kazi cha kufanya uchambuzi wa namna bora ya kutambuamaslahi ya wafanyakazi kupitia bajeti kuu ya serikali ya mwaka 2019/2020. Uchambuziumejikita zaidi katika masuala yote yahusuyo uandaaji wa bajeti yakiwemo sera, sheriakanuni na miongozo mbalimbali, vyanzo vya mapato, uwiano wa mapato na matumizikisekta na mengine. Lengo kuu la uchambuzi huu ni kupendekeza njia nzuri yakumnufaisha mfanyakazi bila kuathiri mwenendo mzima wa uendeshaji wa nchiTumejaribu kutafakari kidogo mambo makuu manne ambayo Baba wa Taifa letutukufu alibainisha kuhusu maendeleo ya taifa lolote. Katika mambo hayo manne,tunapaswa kujiuliza tumepatia wapi, tumekosea wapi au tunakosa nini zaidi na ni ninicha kuongeza. THTU imetafakari na kuongeza jambo moja ambalo tunadhani linafaakatika kuongoza harakati za kufikia Tanzania ya viwanda na hatimae uboreshaji wamaslahi ya wafanyakazi. Mambo hayo kwa muhutasari ni;a) Ardhi - tuna ardhi ya kutosha yenye kila aina ya rasilimali kuliko nchi nyingi zaAfrika. Urasimishaji na mipango bora ya ardhi ni muhimu katika ukuaji wasekta mbalimbali kama vile kilimo, uvuvi na ufugaji ambazo mazao yatokanayona sekta hizo yanachangia ukuaji wa viwanda katika kufikia lengo la nchi lauchumi wa kati kufikia 2025.b) Watu - watanzania tuko zaidi ya milioni hamsini kwa sasa. Hii inamaanakwamba watu wapo. Labda tujadili mambo yahusuyo; maarifa, ujuzi, uzalendo,uadilifu, mtazamo, weledi, uchapakazi na mengine kama yanatusaidiakusukuma gurudumu la maendeleo kiufanisi.c) Uongozi bora –kwa maana ya dhamira, uwezo na mikakati ya viongozi wa ngazizote kuonesha njia na maono sahihi kuwaelekeza watu kufikia uchumi wa katilakini kwa kuzingatia misingi ya utawala bora.d) Siasa safi –kwa maana ya sheria, kanuni na miongozo mbalimbali inayoratibuuendeshaji na mwenendo mzimawa siasa ambayo huleta tija na ustawi wakiuchumi na kijamiie) Wanasiasa – inafahamika kwamba wanasiasa wana ushawishi mkubwa katikanchi. Matendo yao, matamshi yao na mienendo yao kwa ujumla yana atharikubwa katika kufikia malengo tarajiwa kiuchumi na umoja wa kitaifa.Kwa kuzingatia mambo hayo manne, tunajifunza kitu kimoja kikubwa ambacho niumuhimu wa kila mmoja kuchangia maendeleo ya nchi katika nafasi yake. Ardhi ndiyoviii

kitu pekee ambacho kinategemea yale mengine matatu. Hivyo basi, THTU imejikitakatika kutoa mchango juu ya uandaaji wa bajeti kuu ya serikali ya mwaka wa fedha2019/2020 kwa njia ya uchambuzi na mapendekezo.ix

1UTANGULIZIWafanyakazi ni wadau muhimu katika kujenga uchumi wa taifa. Kuna uhusiano wakaribu kati ya wafanyakazi na sekta nyingine zote katika uchumi. Kipatokinachopatikana kutoka kwa mfanyakazi aliyeajiriwa au kujiajiri kwa namna moja aunyingine kinagusa na kufika katika maeneo tofauti kwa njia ya wao kukidhi mahitajimbalimbali ya bidhaa na huduma. Mbali na umuhimu wao mkubwa katika taifa,wafanyakazi wa sekta ya umma wamekua na mahitaji ya aina tofauti yanayohusukupanda madaraja, nyongeza ya mishahara na malimbikizo ya aina nyingine. Ilimaslahi ya wafanyakazi yaweze kuboreshwa, ufanisi wa utekelezaji wa bajeti nakuongezeka kwa mapato ya serikali kuna mchango mkubwa kwa wadau wote katikauchumi.Mara zote nia na mwelekeo wa THTU ni daima kujenga, Taifa kwanza. Kwahiyo lengola andiko hili la Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU)ni kuweka wazi uchambuzi mfupi wa mwenendo wa mapato na matumizi, na kushaurikuhusu bajeti ya mwaka wa fedha 2019/20, kupendekeza namna bora ya kuimarisha nakuongeza mapato ya serikali, utekelezaji wa sera ya viwanda, namna TEHAMA namifumo ya kielektroniki inavyoweza kuboreshwa kusaidia ukusanyaji na usimamiziwa mapato kwa njia bora zaidi. Dhamira kubwa ni kuyafanya hayo yote kwa maslahimapana ya taifa, kukuza uchumi ili mwisho wa siku maslahi ya wafanyakazi ambao ninguzo muhimu yaweze kuboreshwa. Lengo la uchambuzi huu, ni kuangalia ni jinsigani hivyo vyote vitakamilishwa kwa maslahi ya wadau wote wa bajeti ya taifa nawanufaike na bajeti hiyo wakati wa utekelezaji wake. Wadau hao ni wakulima,wafanyakazi, wafugaji, wafanyabiashara na wananchi wengine kwa ujumla.2MIONGOZO MIKUU YA MAANDALIZI YA BAJETIMiongoni mwa miongozo inayotumika kutayarisha bajeti ya serikali ni pamoja na Diraya Maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2025, Ilani ya Chama cha Mapinduzi (2015–2020) naMpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/17–2020/21). Hivyo hata kwa mwakawa fedha 2019/20 miongozo hii inatumika. Yafuatayo ni maelezo jinsi hii miongozoinavyotumika katika uandaaji wa bajeti ya serikali:2.1 Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 ilianza kutekelezwa mwaka 2000 ili kuongoza harakatiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii zitakazoiwezesha Tanzania kufikia uchumi wakati na kuondokana na umaskini uliokithiri ifikapo mwaka 2025. Katika kuchambuabajeti kuu ya serikali Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 inaangazia malengo ambayo ni1

kuhakikisha kuwepo kwa jamii iliyoeleimika vema na inayojifunza na kujenga uchumiimara unaoweza kukabiliana na ushindani kutoka nchi nyingine. Ili kutimiza malengohayo, Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za kuboresha viashiria muhimuvya uchumi kama vile kuchochea ukuaji wa pato la taifa, kushusha mfumuko wa bei,kuvutia wawekezaji wa ndani na nje, kupunguza ukosefu wa ajira pamoja nakuendeleza sekta mbalimbali za kijamii na kiuchumi.Mpango elekezi wa Maendeleo ya Taifa wa Miaka 15: Mpango huu ni muhimu katikautekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 kwa kuwa umeweka wazi mwelekeowa kimkakati kwa muda mrefu na nguzo kuu kwa umakini zaidi, uratibu na kuoanishamipango iliyowekwa ili kuleta maendeleo. Utekelezaji wa mpango huu unafanyikakatika vipindi vitatu: kipindi cha kwanza (2011/12-2015/16) kilihusu uboreshaji wamiundo mbinu ya usafiri, nishati na maji, kilimo, viwanda, maendeleo ya rasilimaliwatu na huduma za jamii, kipindi cha pili (2016/17–2020/21) kinabeba dhana yauchumi unaotegemea viwanda; na kipindi cha tatu (2021/22–2025/26) kinahusuongezeko la ushindani kuwezesha bidhaa zinazozalishwa kuuzwa nje ya nchi.Tunashauri serikali kupitia bajeti ya 2019/20 iendelee kutoa kipaumbele kwenyeupatikanaji wa maji vijijini na kukiwezesha kilimo cha umwagiliaji; nishati endelevukama umeme wa nguvu za jua na upepo; kujenga na kuimarisha miundombinu yamaghala yenye sifa ya kuhifadhi vyakula katika ubora unaostahili; kuweka uwianomzuri kati ya aina ya viwanda vinavyoanzishwa na rasilimali watu wanaozalishwaau/na kuendelezwa na taasisi zetu za elimu na mafunzo. Ni vyema viwanda hivyovikagusa sekta za kitaifa zinazotegemewa na watanzania wengi kama kilimo, ufugaji nauvuvi.2.2 Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2015–2020Ilani hii iliandaliwa kwa kuzingatia Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025 na Mwelekeowa Sera za CCM zenye lengo na nia ya kuendelea kuwatumikia wananchi kwa kipindicha miaka mitano (2015-2020). Vipaumbele vya ilani ni pamoja na: ustawi wa wananchi;kuiwezesha nchi kupata mafanikio makubwa katika nyanja za kiuchumi, kisiasa nakijamii; kuondoa umaskini na kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira hasa kwa vijana.Bajeti ya mwaka wa fedha 2019/20 iendelee kuangazia mambo muhimu yaliyopokwenye ilani kama vile: kuongeza kasi ya kupima maeneo ya wakulima, wafugaji nawavuvi pamoja na kuwapatia hati miliki za kimila ambazo watazitumia kama dhamanaya kuwawezesha kupata mikopo ya kuendeleza shughuli zao za kilimo, ufugaji, uvuvina nyinginezo; kuongeza kasi ya kurasimisha biashara na kuwapatia wafanyabiasharawadogo maeneo ya kufanyia biashara, leseni na fursa za kupata mikopo yenye masharti2

nafuu; na kuanzisha ajira kwa vijana kupitia sera ya viwanda vyenye fursa kubwa zaajira.2.3 Mpango wa Maendeleo wa TaifaMpango huu wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/17–2020/21) unatekelezwa kwakufuata utaratibu wa mwaka mmoja mmoja. Mpango una malengo na vipaumbelekama ifuatavyo kufikia 2020/21: ukuaji wa uchumi (kufikia asilimia 10); mfumuko wabei (wastani usiozidi asilimia 5); udhibiti wa ukuaji wa deni la taifa; udhibiti wa sarafudhidi ya fedha kuu za kigeni (mfano TZS 2,185.62/1 isizidi ifikapo mwaka 2020/21);viwango nafuu vya riba kwa sekta binafsi; urari wa biashara na ukuaji wa sekta yakilimo.Takwimu zinaonyesha malengo ya ukuaji wa uchumi ni asilimia 10 kufikia mwaka2020/21. Hatua ya lengo hili mpaka sasa ni asilimia 7.1 (2016/17) na asilimia 7.2(2017/18). Suala la majadiliano ni uhalisia wa ukuaji wa uchumi kwa mtu mmojammoja ikilinganishwa na ukuaji wa uchumi kitaifa. Ni vyema ukuaji wa uchumi wataifa ulinganishwe na ukuaji wa kipato na maendeleo ya mwananchi wa kawaida.Watanzania wengi (zaidi ya asilimia 65) wanajishughulisha na kilimo, ufugaji na uvuvi.Ili utekelezaji wa awamu ya pili ya kuendeleza sekta ya kilimo (ASDP II) na maeneomengine ya kipaumbele ufanyike kwa ufanisi sekta hizi zipewe kipaumbele katikabajeti ya serikali ya mwaka wa fedha 2019/20.Kuhusu udhibiti wa mfumuko wa bei kubaki katika lengo kuu la wastani usiozidiasilimia 5 (ifikapo 2020/21), mfumuko wa bei kwa mwaka 2016/17 ulikuwa asilimia 5.3na kupungua hadi asilimia 4.3 kwa mwaka 2017/18, ambapo inaonekana hali ni nzurikwa kubakia tarakimu moja1. Serikali iendelee kuimarisha jitihada za kuangalia maeneoyanayosababisha mfumuko wa bei kama vile bei ya mafuta, sera za fedha na bidhaanyingine muhimu zinazoagizwa kutoka nje ya nchi, kama vile chakula na madawa.Udhibiti wa mafuta kwa kufuata bei elekezi inayolingana na soko la dunia itadhibitimfumuko wa bei. Serikali ihakikishe vyakula na madawa yanayoweza kuzalishwa nakuongezwa thamani hapa nchini vizalishwe na kuimarisha uwepo wa kutosha katikasoko la ndani. Udhibiti wa sera za fedha ni muhimu ili kutunza thamani ya fedha nakuchochea ukuaji wa uchumi kama vile kudhibiti matumizi ya fedha za kigeni kwamatumizi yasiyo ya lazima.1Chanzo cha taarifa zote ni Wizara ya Fedha na Mipango.3

Deni la taifa limeongezeka kwa asilimia 39.4 ya pato la taifa kutoka Juni 2017 mpakaJuni 2018 kutokana na serikali kuendelea kukopa ili kugharamia bajeti kuu ya nchi.Serikali iangalie uwezekano kupitia bajeti ya mwaka wa fedha 2019/20 kuwekautaratibu wa kulipa madeni ya ndani na nje; pamoja na, madeni ya wakandarasi wandani, malimbikizo ya stahiki mbalimbali ya wafanyakazi wa umma. Inashauriwaukopaji utakaofanyika kwa mwaka wa fedha 2019/20 uwe kwa ajili ya miradi yamaendeleo na inayoleta tija kwa taifa.Takwimu zinaonyesha viwango vya riba vinaimarika japo taasisi nyingi za kifedhazinakopesha zaidi sekta binafsi zinazojihusisha na biashara; na kwa kiwango kidogokwenye uwekezaji wa viwanda huku sekta za kilimo, ufugaji na uvuvi zinazoajiriwatanzania wengi zikikosa huduma za kifedha na mikopo kwa kiasi kinachoridhisha.Ili kuwezesha ukuaji wa sekta binafsi na u

MUHTASARI Wafanyakazi ni wadau muhimu katika kujenga uchumi wa taifa. Kuna uhusiano wa . Chama cha wafanyakazi wa taasisi za elimu ya juu Tanzania (THTU) kimeanzishwa . yakitokea katika uendeshaji wa vyama hivi na kupelekea kupungua kwa utamaduni wa kutoaminiana uliokuwepo awali. Kutokana na mabad