Sera Ya Elimu Na Mafunzo - Tanzania

1y ago
716 Views
176 Downloads
1.38 MB
77 Pages
Last View : Today
Last Download : 10d ago
Upload by : Victor Nelms
Transcription

Sera ya Elimu na MafunzoSERA YA ELIMU NA MAFUNZO2014i

Sera ya Elimu na Mafunzoii

Sera ya Elimu na MafunzoYALIYOMOVIFUPISHOvDIBAJIviiSURA YA KWANZA11.0. UTANGULIZI11.1. Hali Ilivyo8SURA YA PILI182.0. UMUHIMU WA SERA182.1. Dira, Dhima na Malengo ya Sera19SURA YA TATU213.0. HOJA NA MATAMKO YA SERA3.1. Mfumo, miundo na taratibu nyumbufu kumwezeshaMtanzania kujiendeleza kwa njia mbalimbali katikamikondo ya kitaaluma na kitaalamu21213.2. Elimu na mafunzo yenye viwango vya uboraunaotambulika kikanda na kimataifa na kukidhimahitaji ya maendeleo ya Taifa243.3 Upatikanaji wa fursa mbalimbali za elimu namafunzo nchini3.4. Mahitaji ya Rasilimaliwatu kulingana na Vipaumbelevya Taifa3.5. Usimamizi na uendeshaji madhubuti wa elimu namafunzo nchini3.6. Mfumo endelevu wa ugharimiaji wa elimu namafunzo nchini3.7. Mfumo wa elimu na mafunzo unaozingatiamasuala mtambuka.4046505557iii

Sera ya Elimu na MafunzoURA YA NNE4.0.MUUNDO WA KISHERIA4.1.Utangulizi4.2.Sheria za kusimamia elimu na mafunzoSURA YA TANO5.0.MUUNDO WA KITAASISI5.1.Utangulizi5.2.Ngazi ya Taifa5.3.Ngazi ya Mkoa5.4.Ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa5.5.Ngazi ya Kata5.6.Ngazi ya Shule na Vyuo5.7.Ufuatiliaji na 8

Sera ya Elimu na MafunzoVIFUPISHOIGC-POPCAsasi za KiraiaContinuous AssessmentInternational Growth Centre – Presidents’Office Planning CommissionMKUKUTAMkakati wa Kukuza Uchumi na KupunguzaUmaskini TanzaniaMMEMMpango wa Maendeleo ya Elimu ya MsingiMMESMpango wa Maendeleo ya Elimu yaSekondariMMEJUMpango wa Maendeleo ya Elimu ya Elimu yaJuuMMEUMpango wa Maendeleo ya Elimu ya UfundiMEMKWAMpango wa Elimu ya Msingi kwa WatotoWalioikosaMUKEJAMpango wa Uwiano kati ya Elimu ya WatuWazima na JamiiOWMTAMISEMIOfisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa naSerikali za MitaaSADCSouthern Africa Development CommunityTEHAMATeknolojia ya Habari na MawasilianoUNESCOUnited Nations Educational, Scientific andCultural OrganisationUKIMWIUpungufu wa Kinga MwiliniURTUnited Republic of TanzaniaWyEMUWizara ya Elimu na Mafunzo ya UfundiVVUVirusi vya UkimwiAZAKICAv

Sera ya Elimu na Mafunzovi

Sera ya Elimu na MafunzoDIBAJISerikali imekusudia kuleta mapinduzi ya kiuchumi ili kuibadiliTanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.Sekta ya elimu na mafunzo, kwa mujibu wa Dira ya Maendeleoya Taifa ya 2025 na Mpango wa muda mrefu wa Maendeleoya Taifa 2011/12 hadi 2024/25, inatarajiwa kuleta maendeleoya haraka ya rasilimaliwatu kwa kutayarisha idadi ya kutoshaya Watanzania walioelimika na kupenda kujielimisha zaidi ilikulifanya Taifa lipate maendeleo na kuwa lenye uchumi wa katina shindani ifikapo mwaka 2025. Ili kufikia lengo hili, mfumowa elimu na mafunzo unaotumika nchini lazima utoe fursa zakutosha kwa watu kujielimisha. Hali kadhalika, mfumo huuunawajibika kutoa elimu na mafunzo yenye ubora unaokubalikana kutambulika kitaifa, kikanda na kimataifa. Katika kufanikishahili, Serikali imekuwa ikitekeleza sera mbalimbali, hususan,Sera ya Elimu na Mafunzo (1995), Sera ya Elimu ya Ufundi naMafunzo (1996), Sera ya Taifa ya Elimu ya Juu (1999) na Sera yaTeknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa Elimumsingi (2007)na kuwa na mafanikio mbalimbali. Hata hivyo, katika kipindihicho, changamoto mbalimbali zimejitokeza zikiwemo udhaifukatika mfumo wa elimu na mafunzo, uhaba wa walimu, uhabawa zana, nyenzo na vifaa na miundombinu ya kufundishia nakujifunzia pamoja na changamoto katika ithibati na uthibitiwa ubora wa shule na vyuo katika ujumla wake vimechangiakatika kushuka kwa ubora wa elimu na mafunzo nchini.Sera hii imebainisha masuala ambayo Serikali, kwakushirikiana na wadau katika elimu na mafunzo,itayawekea mkazo zaidi ili kuweka mazingira mazuriya kufikia malengo ya mipango ya maendeleo. Masualahaya ni pamoja na kuinua ubora wa mfumo wa elimu navii

Sera ya Elimu na Mafunzomafunzo ili uwe na tija na ufanisi, kuendelea kutoa fursa zaelimu na mafunzo kwa usawa na kuendelea kuinua uborawa mitaala ya elimu na mafunzo ili ikidhi mahitaji yamaendeleo ya Taifa. Aidha, Serikali itaendeleza matumiziya lugha ya Kiswahili, Kiingereza, Alama, pamoja na lughanyingine za kigeni katika elimu na mafunzo. Vilevile,itaendelea kuinua ubora wa mfumo wa upimaji, tathminina utoaji vyeti katika ngazi zote. Serikali itaimarisha uwezowa uongozi na utawala katika sekta ya elimu na mafunzona kupanua wigo wa ugharimiaji wa elimu na mafunzo.Sera hii mpya inaweka Dira ya elimu na mafunzo nchinikuwa ni “Mtanzania aliyeelimika na mwenye maarifa, stadi,umahiri, uwezo na mitazamo chanya ili kuweza kuchangia katikakuleta maendeleo ya Taifa” na Dhima yetu kuwa ni “kuinuaubora wa elimu na mafunzo na kuweka mifumo na taratibuzitakazowezesha kupata idadi kubwa ya Watanzania walioelimikana wanaopenda kujielimisha zaidi ili waweze kuchangia katikakufikia malengo ya maendeleo ya Taifa letu”. Ili kufanikishautekelezaji wa Sera hii kwa ukamilifu, kunahitajikaushiriki wa wadau wote wa elimu na mafunzo katikangazi zote, ikiwemo sekta binafsi, Asasi za Kiraia (AZAKI)na washirika wengine wa maendeleo.Mwisho, napenda kuwashukuru wale wote walioshirikikwa namna moja au nyingine katika mchakato mzima wakukamilisha Sera hii.Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa (Mb)Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundiviii

Sera ya Elimu na MafunzoSURA YA KWANZA1.0.UtanguliziSera hii ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 ni matokeo yakuhuishwa na hatimaye kufutwa kwa Sera ya Elimu na Mafunzo(1995), Sera ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo (1996), Sera yaTaifa ya Elimu ya Juu (1999) na Sera ya Teknolojia ya Habari naMawasiliano kwa Elimu Msingi (2007). Utekelezaji wa Sera yaElimu ya Ufundi na Mafunzo (1996) na Sera ya Taifa ya Elimuya Juu (1999) ulisimamiwa na iliyokuwa Wizara ya Sayansi,Teknolojia na Elimu ya Juu; na utekelezaji wa Sera ya Elimu naMafunzo (1995) na Sera ya Teknolojia ya Habari na Mawasilianokwa Elimu Msingi (2007) ulisimamiwa na iliyokuwa Wizaraya Elimu na Utamaduni. Mwaka 2006, Serikali ilibadilishamuundo wa iliyokuwa Wizara ya Elimu na Utamaduni kuwaWizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kujumuisha elimuya juu na baadaye mwaka 2008 kujumuisha elimu ya ufundikatika wizara hiyo. Sera hizo za elimu, kwa ujumla, zilitoamwongozo kuhusu kuongeza ushirikishwaji wa sekta binafsi;kuongeza fursa za elimu na mafunzo kwa usawa; kupanuawigo wa ugharimiaji wa elimu na mafunzo; kuhuisha muundowa uongozi wa elimu kwa kupeleka madaraka na majukumukatika ngazi ya shule, jamii, wilaya na mikoa; kuinua ubora waelimu; kuimarisha uhusiano kati ya elimu rasmi na elimu nje yamfumo rasmi na kuwezesha ukuaji wa utamaduni wa elimu yakujiajiri na kubuni ajira.Katika miaka 19 ya utekelezaji wa Sera ya kwanza ya Elimu naMafunzo ya mwaka 1995 pamoja na Sera nyingine mahususiza elimu na mafunzo, Tanzania imepata mafanikio makubwakatika sekta ya elimu. Mafanikio haya ni pamoja na kupanuawigo wa elimu katika ngazi zote, kuanzia elimu ya awali hadi1

Sera ya Elimu na Mafunzoelimu ya juu. Kwa mfano, kwa kutumia taarifa zilizopo za miakambalimbali, idadi wa watoto wanojiunga na elimu ya awaliimeongezeka kutoka asilimia 24.7 mwaka 2004 hadi 37.3 mwaka2013 na kiwango cha watoto walioandikishwa katika elimu yamsingi imeongezeka kutoka asilimia 77.6 mwaka 1995 hadiasilimia 96.2 mwaka 2013. Kiwango cha watoto wanaojiungana elimu ya sekondari kimeongezeka pia kutoka asilimia 14.6mwaka 1995 hadi 59.5 mwaka 2013.Hali kadhalika, idadi ya wanafunzi wanaojiunga na elimu yaufundi na mafunzo ya ufundi stadi imeongezeka kutoka 4,641mwaka 2000/01 hadi 145,511 mwaka 2012/13. Aidha, elimu yajuu imepanuka ambapo vyuo vikuu na vyuo vikuu vishirikivimeongezeka kutoka chuo 1 mwaka 1995 hadi 50 mwaka 2013na kuwezesha idadi ya wanafunzi wanaojiunga na elimu yajuu kwa ngazi ya Shahada kuongezeka kutoka 16,727 mwaka2000/01 hadi 162,510 mwaka 2012/13.Utekelezaji wa Sera za Elimu na Mafunzo ulifanyika kupitiasheria, kanuni, miongozo pamoja na Programu ya Maendeleoya Sekta ya Elimu iliyoandaliwa mwaka 1997. Kupitia programhiyo, uliandaliwa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi(MMEM), Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari(MMES), Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Juu (MMEJ)na Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo(MMEU). Pia kulikuwa na mipango na programu mbalimbalikwa ajili ya maendeleo ya elimu ya watu wazima na elimunje ya mfumo rasmi. Kupitia sheria, kanuni, miongozo namipango hii, fursa za elimu na mafunzo zimeongezeka katikangazi zote; ugatuaji wa majukumu katika sekta ya elimu namafunzo umefanyika kutoka Serikali Kuu kwenda Mamlaka zaSerikali za Mitaa; vyombo vya ithibati na uthibiti wa ubora wa2

Sera ya Elimu na Mafunzoelimu na mafunzo ya ufundi, elimu ya vyuo vikuu, mfuko waelimu na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu piavimeanzishwa na vinafanya kazi nzuri ya kuendeleza elimu namafunzo nchini.Hata hivyo, changamoto nyingi zimejitokeza katika kipindi chautekelezaji wa Sera hizi, ambazo zimekuwa zikiathiri uborana usawa katika elimu inayotolewa kwenye ngazi mbalimbali.Changamoto hizi ni pamoja na upungufu wa miundombinu navifaa vya kufundishia na kujifunzia ikiwemo vitabu, maabara,maktabana madarasa;. upungufu wa walimu hususan walimuwa sayansi, hisabati na stadi za kusoma, kuhesabu na kuandika;kushuka kwa morali ya kufundisha miongoni mwa walimu kwasababu ya maslahi yasiyoridhisha na mazingira magumu yakazi; utambuzi hafifu wa wanafunzi wenye mahitaji maalumuna mazingira duni ya kujifunzia; kutokuwepo kwa utaratibu wautambuzi na uendelezaji wa wanafunzi wenye vipaji na vipawa;matumizi hafifu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA) katika utoaji wa elimu na mafunzo; na walimu nawanafunzi kutomudu lugha ya kufundishia na kujifunzia katikangazi mbalimbali za elimu. Vilevile kiwango cha watu wazimawenye kufahamu kusoma, kuandika na kuhesabu kimeshukakutoka asilimia 85 mwaka 1992 hadi asilimia 77.9 kulingana naSensa ya Taifa ya mwaka 2012.Aidha, bado Sekta ya elimu na mafunzo inakabiliwa nachangamoto ya mfumo usiokidhi mahitaji ya elimu namafunzo nchini. Mfumo wa elimu na mafunzo umetawaliwana muundo wa kitaaluma wenye dhana ya kuchuja wahitimuili kupata wachache wenye uwezo mkubwa katika taaluma nawatakaosoma hadi kumaliza katika ngazi ya chuo kikuu. Halihii inatokana na nafasi za elimu na mafunzo ngazi za juu kuwa3

Sera ya Elimu na Mafunzochache kadri wanafunzi wanavyohitimu kuanzia ngazi ya elimuya msingi na kuendelea, hivyo kuwa na muundo wa kuchujabadala ya ule wa kutoa fursa kulingana na uwezo, vipaji navipawa. Hali kadhalika, muundo wa 2 7 4 2 3 unachukuajumla ya miaka 18 kutoa rasilimaliwatu. Hii ina maana kwambamwanafunzi anayeanza masomo akiwa na umri wa miaka 7atamaliza elimu ya juu akiwa na umri wa takribani miaka 23.Umri huu ni mkubwa ikilinganishwa na nchi nyingine kama zaAfrika ya Kusini, Maurishasi, Malesia na Ufini ambapo umri wakijana anayemaliza elimu ya juu ni takribani miaka 20 hadi 22.Vilevile, hakuna mwingiliano fanisi kati ya muundo wa elimuya ufundi na muundo wa elimu ya jumla na hivyo kushindwakuwawezesha wahitimu wa elimu ya ufundi kujiendelezakatika elimu ya juu. Pamoja na hayo, kuna ukosefu wa mfumoendelevu wa utambuzi wa sifa mbadala utakaowawezeshawatu waliopata ujuzi kwa njia mbalimbali za elimu na mafunzokujiendeleza kielimu na kuingia katika ulimwengu wa kazi.Vilevile, kumekuwa na changamoto katika kuinua uborawa elimu na mafunzo kutokana na mitaala katika ngazimbalimbali za elimu na mafunzo kutokidhi mahitaji yamabadiliko ya kiuchumi, kijamii, kisayansi na teknolojia nahivyo kutoa wahitimu ambao hawana umahiri wa kutoshakuhimili ushindani katika ulimwengu wa kazi. Aidha,Taasisina mashirika yanayotoa huduma za kielimu yaliyopo chini yaWizara yenye dhamana ya elimu na mafunzo yana mamlakakamili ya uendeshaji wa shughuli za elimu bila kuwa namahusiano ya kisheria katika utendaji baina yao na wizarazinazosimamia elimu na mafunzo na hivyo kuathiri uborawa elimu itolewayo. Hali kadhalika, changamoto nyingine nikutokuwepo kwa ugharimiaji endelevu kutokana na mifuko ya4

Sera ya Elimu na Mafunzoelimu kutokidhi mahitaji ya elimu katika ngazi zote na hivyokuhitaji vyanzo vingine vya ugharimiaji endelevu wa elimu namafunzo.Utekelezaji wa Ibara ya 146(1) ya Katiba ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania (1977) kuhusu ugatuaji umekuwa nachangamoto mbalimbali. Katiba inatamka katika Sura ya Nane(kuhusu madaraka kwa umma), kwamba, madhumuni yakuwapo Serikali za Mitaa ni kupeleka madaraka kwa wananchina hivyo kuwezesha Serikali za Mitaa kuwajibika kutekelezakazi zake katika eneo husika. Sheria za Serikali za Mitaa zinatoamajukumu kwa Halmashauri kuhusu elimu katika Kifungu cha55 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka ya Miji) ya 1982. Nikwa mantiki hii, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniakupitia Matangazo ya Serikali Na. 494 na 494A ya mwaka 2010aligatua na kuiweka katika usimamiaji wa OWM-TAMISEMIelimu ya awali, msingi na sekondari na kuacha Wizara ya Elimuna Mafunzo ya Ufundi kushughulikia Sera katika masuala yoteya elimu na mafunzo. Hata hivyo bado kuna changamoto zamuingiliano wa baadhi ya majukumu katika utekelezaji waugatuaji kwa upande wa utendaji na usimamiaji wa elimu kati yaWizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na OWM-TAMISEMI.Katika miaka ya hivi karibuni, viwango vya ubora wa elimuvimekuwa vikishuka. Hali hii inadhihirishwa na ufaulu katikamitihani ya kuhitimu elimu ya msingi na elimu ya sekondaringazi ya kawaida kuwa na mserereko wa kushuka kutokaasilimia 54 mwaka 2007 hadi kufikia asilimia 31 mwaka 2012,kwa upande wa elimu ya msingi; na asilimia 90 mwaka 2007hadi asilimia 43 mwaka 2012 kwa elimu ya sekondari; wakatiidadi ya watahiniwa inaongezeka mwaka hadi mwaka.Maarifa na Ujuzi wa wahitimu katika ngazi hizo ni mdogo5

Sera ya Elimu na Mafunzoikilinganishwa na ngazi ya elimu waliyofikia. Hali kadhalika,maarifa na ujuzi wa wahitimu wa mafunzo ya ufundi na elimuya juu havikidhi mahitaji mbalimbali katika ulimwengu wa kazi.Tathmini zinaonyesha kwamba, ili kuimarisha ubora na ufanisiwa elimu na mafunzo nchini, kuna ulazima wa kuimarishamaeneo mbalimbali ambayo yanahusika na ubora wa elimu namafunzo.Katika harakati za kimaendeleo, yapo mabadiliko ya sera zakijumla na mipango ya kitaifa iliyojitokeza katika kipindicha utekelezaji wa sera hizi. Kutokana na Dira ya Taifa yaMaendeleo 2025 na Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Mudamrefu 2011/12 hadi 2024/25, Serikali imelenga kujenga jamiiiliyoelimika na yenye kupenda kujielimisha. Pamoja na azmahiyo, Tanzania imeridhia Itifaki ya SADC (1997) kuhusu elimuna mafunzo inayozitaka nchi wanachama kuwa na elimumsingiya lazima kwa kipindi kisichopungua miaka tisa; Itifaki ya Dakar(2000) kuhusu Elimu kwa wote; Makubaliano ya Perth UNESCO(2007) kuhusu Elimu ya Sayansi na Teknolojia na mafunzo yaufundi na mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Aidha,kuna baadhi ya masuala mtambuka yakiwemo mazingira,jinsia, VVU na UKIMWI na Ubia baina ya Sekta ya Umma naSekta Binafsi ambayo yamejitokeza na yanahitaji kujumuishwakatika Sera ya Elimu na Mafunzo.Sekta ya elimu na mafunzo ina jukumu la kuandaa na kuzalisharasilimaliwatu kwa ajili ya Taifa. Ripoti mbalimbali zinaonyeshakwamba kuna nakisi kubwa ya wataalamu walioelimika kwakiwango cha elimu ya juu wanaohitajika ili Tanzania ifikie kuwanchi yenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. Taarifa ya IGCPOPC (2011) inaonyesha kuwa, Rasilimaliwatu ya Tanzania,kwa kiasi kikubwa, ni wafanyakazi wenye ujuzi wa chini ambao6

Sera ya Elimu na Mafunzoni asilimia 84, wakifuatiwa na wenye ujuzi wa kati ya asilimia13 na wenye ujuzi wa juu asilimia 3. Hata hivyo, kwa nchi zakipato cha kati ngazi ya chini, ulinganifu unaonyesha kuwanchi hizo zina wastani wa asilimia 55 ya wafanyakazi wenyeujuzi wa chini, asilimia 33 ujuzi wa kati na asilimia 12 ujuziwa juu. Hivyo, sekta ya elimu na mafunzo ina changamoto yakuinua mchanganyiko wa wafanyakazi wenye ujuzi katika fanimbalimbali ili kufikia mahitaji ya rasilimaliwatu kwa nchi yakipato cha kati ifikapo mwaka 2025.Mfumo wa elimu na mafunzo wa sasa una changamotoya kuliwezesha Taifa kukidhi ongezeko la mahitaji yarasilimaliwatu kulingana na vipaumbele vya Taifa kwa sababutakwimu za elimu za mwaka 2000 hadi 2012, zinaonyesha kuwani wastani wa asilimia 5 tu ya wahitimu wa darasa la saba ndiyowanaofaulu na kuendelea hadi kufikia elimu ya sekondari yajuu; na wastani wa asilimia 4 tu ya wahitimu hao wa darasa lasaba ndiyo wanaofaulu na kuendelea hadi elimu ya juu. Kwamwenendo huo ni dhahiri kwamba Taifa litaendelea kuwa nanakisi ya wataalamu kama hatua madhubuti za kuongeza fursana kuinua ubora wa elimu hazitachukuliwa.Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 imeandaliwa ilikutoa mwelekeo wa elimu na mafunzo nchini kwa kuzingatiamabadiliko ya kiuchumi, kijamii, kisayansi na kiteknolojia nachangamoto za elimu na mafunzo kitaifa, kikanda na kimataifa,ili kuongeza fursa, ufanisi na ubora wa elimu na mafunzo nchinina kufikia viwango vya rasilimaliwatu kwa nchi yenye uchumiwa kati ifikapo mwaka 2025.7

Sera ya Elimu na Mafunzo1.1.Hali IlivyoUchambuzi wa tathmini ya utekelezaji wa Sera ya Elimuna Mafunzo ya mwaka 1995, umeonyesha kuwa matamko59 kati ya matamko 149 ya Sera hayakutekelezwa. Kati yahayo, matamko 25 yalihusu elimu ya msingi na sekondari,18 yalihusu elimu ya ufundi na 16 yalihusu elimu ya juu.Tathmini ilibaini pia kuwa mpango mkakati wa kuelekezautekelezaji wa sera hizo haukuandaliwa mpaka mwaka 1997ulipoanzishwa Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu, namwaka 2001 ulipoandaliwa Mpango wa Maendeleo ya Elimuya Msingi (MMEM). Tathmini ilibaini pia kuwa usimamizina uendeshaji wa elimu na mafunzo katika ngazi ya mkoa nawilaya unafanywa na mamlaka mbalimbali zinazoongozwana kanuni na taratibu tofauti pamoja na OWM-TAMISEMI.Walimu wanaandaliwa na kuajiriwa na Wizara ya Elimu naMafunzo ya Ufundi wakati haki zao za kiutumishi na nidhamuzinashughulikiwa na Idara ya Utumishi wa Walimu. Utaratibuhuu wa usimamizi wa walimu chini ya mamlaka tatu tofautiunafanya hali ya uwajibikaji na utawala bora kuwa mgumu.Kutokana na taarifa ya tathmini, inapendekezwa kuwa Serikaliiunde Bodi ya kitaalamu ya kusimamia maendeleo ya utaalamuwa ualimu. Vilevile walimu wawe chini ya mwajiri mmojaatakayeshughukia masuala ya ajira, nidhamu na maendeleoyao.Vyuo vya elimu ya ufundi stadi na vyuo vya ualimuhavikuwekewa muundo wa kitaasisi unaoviunganisha namaafisa elimu wa wilaya na mikoa kama ilivyoelekezwa kwenyeSheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978 na katika Sera ya Elimuna Mafunzo ya mwaka 1995. Taasisi zilizo chini ya Wizarazinazotoa huduma za kielimu hazina uhusiano wa kiutendaji8

Sera ya Elimu na Mafunzokatika utekelezaji wa majukumu yao kati ya taasisi na taasisi nauhusiano wa moja kwa moja na Wizara ya Elimu na Mafunzoya Ufundi pamoja na OWM-TAMISEMI. Katika tathmini hiyoilipendekezwa kuwa kiundwe chombo kitakachokuwa nawajibu wa kuratibu na kuhakiki ubora wa mitaala, upimaji,utoaji vyeti na tuzo, ithibati na uthibiti wa ubora wa elimu yamsingi na sekondari.Uchambuzi wa tathmini hiyo ulibaini kwamba kuna umuhimuwa kupunguza miaka ya kupata elimu ya awali kutoka miakamiwili hadi mwaka mmoja, na kupunguza umri wa kuanzadarasa la kwanza kuwa miaka mitano badala ya miakasaba. Muundo wa elimu wa sasa wa 2 7 4 2 3 pamoja nakwamba ulionekana kuwa umelisaidia Taifa hadi tulipofikia,huchukua muda mrefu tangu mwanafunzi anapoanza elimu yamsingi mpaka anapohitimu chuo kikuu. Tathmini pia ilibainikuwa elimu inayotolewa katika ngazi ya elimu ya msingi nasekondari imeegemea zaidi kwenye mkondo wa taaluma hivyokupunguza uwezo wa kubaini vipaji na vipawa vya wanafunzina kuviendeleza katika stadi nyingine nje ya taaluma. Tathminihiyo ilipendekeza kuwa na muundo wa 1 6 4 2 3 ambaomhitimu atamaliza mzunguko wa masomo kwa mudamfupi; na mikondo ya ufundi ijumuishwe kwenye elimu yamsingi na sekondari. Utambuzi wa watoto wenye vipaji navipawa ufanyike mapema katika elimu ya awali na msingi iliwaendelezwe katika ngazi zinazofuata.Tathmini pia ilionyesha kuwa mitaala ya baadhi ya vyuohaina ulinganifu katika maudhui na muda wa mafunzo kwaprogramu zinazolingana na kufanana. Aidha, maudhui yamitaala y

wa mitaala ya elimu na mafunzo ili ikidhi mahitaji ya maendeleo ya Taifa. Aidha, Serikali itaendeleza matumizi ya lugha ya Kiswahili, Kiingereza, Alama, pamoja na lugha nyingine za kigeni katika elimu na mafunzo. Vilevile, itaendelea kuinua ubora wa mfumo wa upimaji, tathmini na utoaji vyeti katika ngazi zote.